Tuesday, January 29, 2013

UCHURO VIFO VYA MASTAA

 
 Na George Kayala
KATIKA hali ya kuendeleza uchuro unaofanywa na mastaa mbalimbali, msanii wa sinema za Kibongo, Jacqueline Pentzel ‘Jack Chuz’ (pichani) hivi karibuni ametoa mwongozo wa mazishi yake yatakavyokuwa pindi akifariki dunia, Risasi Jumamosi linakubainishia.
RANGI YA JENEZA
Jack amesema kuwa anapenda jeneza lake lipambwe kwa rangi ya fedha (silver) kwani anaipenda sana rangi hiyo.
“Japokuwa wakati huo sitakuwa nikijua kinachoendelea, naomba ndugu, jamaa na marafiki zangu wazingatie jambo hilo,” alisema.
NGUO ZA WAOMBOLEZAJI
Pia, staa huyo amepanga nguo vitakazovaliwa na waombolezaji watakaofika katika msiba wake ziwe za rangi ya pinki na nyeupe.
“Nawaomba ndugu na marafiki zangu wa karibu siku hiyo washone nguo zenye rangi nyeupe na pinki. Rangi nyeupe inawakilisha amani, japokuwa nitakuwa nimekufa, nitapenda kila mmoja abaki na amani kwani kila nafsi itaonja mauti.”
KWA NINI PINKI?
Jack amesema kuwa anaipenda rangi ya pinki na siku hiyo itakuwa inawakilisha upendo kwani yeye ni mtu wa upendo kwa kila mtu.
“Pamoja na kwamba sitakuwa najua kinachoendelea ulimwenguni lakini suala la upendo kwa kila mmoja ni la muhimu. Hivyo, nitapenda ndugu zangu waishi kwa upendo kwani hiyo ni amri kuu ya Mungu ambayo aliagiza tupendane.”
JIDE
Hata kabla ya mwaka haujakatika, msanii wa Bongo fleva, Judith Wambura ‘Jide’ naye aliweka wazi jinsi anavyotaka watu wavae siku ya mazishi yake.
Mbali na hivyo, Jide alitoa hadi mfano wa jeneza analotaka azikwe nalo.
JACK PATRICK NAYE
Naye mwanamitindo, Jacqueline Patrick hakubaki nyuma, alichukua fursa kueleza jinsi atakavyopenda azikwe baada ya kukata roho

No comments:

Post a Comment