Monday, April 23, 2012








Ephraim Kibonde.

Na Luqman Maloto

UCHAKUBIMBI ni tabia, ikiendekezwa inaweza kuwa ugonjwa wa kudumu. Ukizoea sana kuwa mropokaji, kushabikia mambo yasiyo na faida, halafu vitu vya msingi vyenye sura ya maendeleo ukavipa kisogo, hayo ni maradhi mabaya. Yanaingia mpaka akilini. Huo ni uchakubimbi.

Asili ya chakubimbi ni kusema uongo bila kipimo, hana rafiki, anamfitinisha kila aliye karibu naye. Sifa yake nyingine ni kizabizabina anayezungumza na kusherehesha mambo hata asiyoyajua. Anawachukia walio mbali naye, anawafanyia husuda hata waliopo…

Asili ya chakubimbi ni kusema uongo bila kipimo, hana rafiki, anamfitinisha kila aliye karibu naye. Sifa yake nyingine ni kizabizabina anayezungumza na kusherehesha mambo hata asiyoyajua. Anawachukia walio mbali naye, anawafanyia husuda hata waliopo karibu na yeye.

Leo nahusika na Mtangazaji wa Clouds FM, Ephraim Kibonde. Sina maana yeye ni chakubimbi au kizabizabina, ila anapenda sana kuropoka na kuzungumza mambo bila kutafakari. Asichofanyia utafiti, yeye atakishabikia na kukizungumza kwa ujasiri mkubwa.

Huu ndiyo ugonjwa mbaya wa Kibonde. Anaishi nao kwa muda mrefu sasa, nalijua tatizo lake kitambo ila nilinyamaza kwa kuvuta subira kwa kuamini kwamba anakua, hivyo hekima itamuongoza. Amebaki kuwa yuleyule, hakui. Ameendelea kuwa mtu mzima mtukutu.

Bahati mbaya zaidi, Kibonde amekuwa sawa na mtu asiyejitambua. Hajui dhima aliyonayo akiwa redioni. Anajifanya hajui matumizi mabaya ya redio athari yake ni nini. Anabwabwaja bila kipimo, anavunja heshima ya Redio ya Watu, Clouds FM.

Mabosi wa Kibonde najua wanalijua hili. Sina shaka kwamba walishapokea malalamiko kutoka kwa watu tofauti kuhusu kinywa cha mfanyakazi wao. Inawezekana wanamvumilia au hawaoni matokeo hasi. Kama kweli hawalioni, nawapa ukweli halisi kuwa anaishambulia redio yao.

Kibonde ni sawa na mchezaji anayeonekana anang’ara uwanjani, anapiga chenga huku na huko, anatoa pasi maridadi na kukaba sana lakini mwisho anajifunga. Clouds FM kama wanaona ni vizuri kuendelea kuwa na mchezaji wa aina hiyo sawa, ni uamuzi wao ila ipo siku watakumbuka maneno haya.

Haya makosa ya kujifunga mara kwa mara ya mchezaji wao Kibonde, yatasababisha ripoti mbaya kitakwimu katika eneo la idadi ya wasikilizaji. Namba ya wasikilizaji inaposhuka ni picha inayojitosheleza kuwa ni athari ya zile pointi zilizopotea kutokana na magoli ya kujifunga.

Hilo ni angalizo lakini ni ukweli usiofichika kuwa Kibonde anaishambulia Clouds FM. Anaharibu heshima ya Kipindi cha Jahazi kwa namna anavyobwatuka mithili ya mtu anayeweweseka usingizini. Linalomjia kinywani yeye twende. Ameshazungumza sana lugha chafu redioni.

Clouds FM wanasahau hata hili? Kibonde ndiye aliyeichonganisha redio hiyo na Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF). Tangu mwaka 2009, Clouds imejitoa kushiriki michuano ya NSSF Media Cup (chanzo ni Kibonde). Alisema uongo, akaichongea kampuni yake.

Hata asilolijua analitolea ufafanuzi; Katika mashindano ya NSSF Media Cup mwaka 2009, ulitokea utata kuhusu mfanyakazi wa Clouds FM anayeitwa Shah. Wakati wa kutafuta uhakika, akaulizwa Kibonde, naye akaruka futi 100 kuwa mtu huyo hafanyi kazi sehemu yeyote katika makampuni ya Clouds.

Alijibu kama anajua vile, kumbe hajui kitu. Asilolijua anajifanya analijua. Akamkana mfanyakazi halali wa Clouds FM kwa kiherehere chake. Akajifanya msemaji wa kampuni wakati hata ajira hana. Katika malumbano ya mfanyakazi huyo, ikatolewa siri kwamba Kibonde si mwajiriwa wa Clouds.

Kumbe yeye ni mtumishi wa muda tu. Lugha rahisi ni deiwaka au kibarua. Siri hii ilibainika kutokana na maelezo ya Mkurugenzi wa Vipindi Clouds Media Group, Ruge Mutahaba, akifafanua uhalali wa Shah kuwa mtumishi wa kampuni yake na kwamba NSSF ilikosea kusikiliza maelezo ya Kibonde kwa sababu siyo mhusika na wala siyo mwajiriwa.

Yaani huyu mtu ni deiwaka au kwa lugha nyepesi kibarua lakini anaropoka, anapandisha mabega utadhani ni mtu mwenye daraja fulani kwenye kampuni. Hata kazi yake ukifuatilia siyo mtangazaji ila yupo kwenye Jahazi kama mshereheshaji wa mada (MC).

Amezoea u-MC, kwa hiyo hajui maadili na miiko ya utangazaji. Mtangazaji anapaswa kuwa mtu mwenye akili timamu. Mtu ambaye ubongo wake unafanya kazi muda wote, kwa hiyo anaweza kuchuja la kuzungumza na kuliacha. Kibonde ana upungufu huu, kila analopokea analitamka hewani.

Ni lazima atambue yeye mwenyewe kuwa anapoteza sifa ya kuwa mtangazaji. Pengeni hata u-MC wa shughuli za heshima hatakiwi. Anachostahili yeye ni ‘dili’ za kusherehesha matukio ya vumbini ambako anaweza kuropoka lolote. Utangazaji ni fani yenye maadili, haimfai.

Labda nitoe mfano: Mke wa Kibonde ana Virusi Vya Ukimwi (VVU), anakwenda kwenye chombo cha habari (nasisitiza huu ni mfano jamani). Anakutana na mwandishi akiwa na vyeti vyake na kujitangaza kwamba yeye ni muathirika wa ugonjwa huo.

Mwandishi anapokwenda kuripoti habari hiyo kwa mhariri wake, kwa sababu za busara za mhariri anaamua kuizuia habari hiyo isiende, kwani kuichapisha maana yake ni kumuathiri na Kibonde. Kuandika kwamba mke anaishi na VVU, wakati mume hajawa tayari kujitangaza ni sawa na unyanyapaa.

Huu ni mfano lakini hizo ndizo busara za kiweledi katika fani ya habari. Ikitokea Kibonde mtu anakwenda kwake anataka kujitangaza anaishi na VVU, hawezi kufikiria upande wa pili kama mhariri alivyofanya, atabwabwaja tu. Anahitaji mafunzo ya ziada ili aache hayo lakini ni faida kwa Clouds FM endapo menejimenti itafikiria mara ya pili.

Mfano mmojawapo wa Kibonde mropokaji ni huu; Wakati wa malumbano ya mgogoro wa haki ya kutekeleza mradi wa malaria mwaka juzi, inaonekana aliamua kulivalia njuga suala hilo, kwa kuamini ndiyo mabosi wake watampenda. Maskini weeee! Aliharibu kupita kiasi.

Unataka kujua alifanya nini? Funua kesho Gazeti la Uwazi.

Chanzo:http://www.globalpublishers.info/

No comments:

Post a Comment