Friday, August 10, 2012

AVUA PETE, AMTOSA MUME WA MTU


Salma Jabu ‘Nisha’.


STAA wa filamu Bongo,  ameamua kuvua pete ya uchumba baada ya kuona anaandamwa na maneno kutoka kwa mwanamke anayedaiwa ni mke wa mwanaume aliyemvisha pete hiyo, Geofrey Kusila.

Akizungumza na Ijumaa hivi karibuni Nisha alisema, yeye ni msanii lakini pia anafuata maadili ya dini ya Kiislam hivyo kutokana na malalamiko ambayo amekuwa akiyatoa mwanamke anayedai kuingiliwa katika penzi, yeye ameamua kujitoa.

“Nilimpenda Geofrey ndiyo maana nikakubali anivalishe pete ya uchumba lakini nimeona bora niachane naye kwani najisikia vibaya ninaposikia yule mwanamke wake ananilalamikia.

“Ukichukulia huu ni Mwezi Mtukufu, ili Mungu aikubali swaumu yangu, bora niachane na mwanaume huyo ili mke wake awe na amani, mimi nitampata mwingine,” alisema…






No comments:

Post a Comment