Beki mpya wa timu ya Yanga kutoka timu ya APR ya Rwanda,Mbuyi Twite akipokea jezi ya yake mpya kutoka kwa Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Yanga,Abdallah Binkrebu.
Akipiga sain kwa dole gumba....... wino tena!!
Always pen ikiwa mwisho...... huku
Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Yanga,Abdallah Binkrebu. akishuhudia Tukio zima
SIKU moja baada ya Mwenyekiti wa Simba Ismail Rage kumtuhumu mtoto wa kigogo kuhusika kuwahujumu katika usajili wa beki wa Rwanda Mbuyi Twite kwa kumsajili kwa mahasimu wao Yanga, uongozi wa Yanga umekuja juu na kumtaka Rage adhibitishe kauli yake ikiwa ni pamoja na kumtaja mtoto huyo wa kigogo.
Rage alitoa kauli hiyo juzi mpaka kumpelekea kumwaga chozi sambamba na kujiudhuru nafasi yake ya Ujumbe wa Kamati ya Katiba,Sheria,Maadili na Hadhi za wachezaji ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kwa madai ya shirikisho hilo kuikandamiza klabu yake.
Akizungumza Makao Makuu ya klabu hiyo Mtaa wa Twiga na Jangwani Katibu Mkuu Yanga,Selestine Mwesigwa alisema kuwa wao wanajua Rage ni muugwana na ni mkubwa katika nchi hii wanajua atamtaja na kuleta vithibitisho juu ya hilo mapema bila ya kuambiwa muda.
Aidha Mwesigwa alitoa ufafanuzi juu ya suala la mchezaji Mbuyu Twite ambaye inasemekana Simba wamemsajili na kusema kuwa wao Yanga wamemsajili kwa kufuata na kuheshimu kanuni na sheria za Cuf,TFF na FIFA hivyo basi wao hawajakurupuka katika usajili wake.
“Wenzetu naweza sema wamekurupuka kwa kuwa hawajafuata sheria wakati ndugu yangu Rage anajua kanuni na Sheria kwa hili namshangaa sana.”alisema Mwesigwa.
Alisema wao wameanza kufanya mchakato wa kumnasa beki huyo toka Novemba mwaka jana kabla ya kuanza mazungumzo na Simba juu ya aliyekuwa beki wao Kelvin Yondan na kusema kuwa walimtuma Mjumbe wa kamati ya Utendaji Abdallah Binkrebu kumfuatilia toka kipindi hicho.
“Sisi huyu mchezaji tumemsaka toka muda mrefu kabla hata ya Kagame kuanza na mara baada ya kumalizika kwa Kagame tulikuwa tunaangalia kiwango chake na kikaturisha.
"Binkrebu akafunga safari na kwenda kuzungumza na uongozi wa timu yake ya Fc Lupopo ya Kongo na wala sio APR, Simba wao wamenunua mali ya wizi wakati sisi tumeenda kwa mwenye mali.
Aliongeza kuwa mara baada ya leo kupeleka majina ya timu yao TFF ndipo wataweka adharani mambo mbalimbali juu ya beki huyo ikiwa na mkataba wake wa kuitumikia klabu hiyo.
|
No comments:
Post a Comment