Staa wa muziki wa Genge Kenya Jua Cali ijumaa iliyopita amepata nafasi kubwa kwenye headlines Kenya baada ya kusambaa kwa picha za gari lake jipya alilonunua aina ya Chrysler crossfire ya 2005 ambalo lina wiki nne tu toka limefika Kenya according to kenyan-post.com
Mwishoni mwa mwaka jana Jua Cali akizungumza exclusive na millardayo.com alisema mikataba ya makampuni mawili ya simu nchini Kenya aliyofanya nayo kazi kwa nyakati tofauti ndio iliyombadilishia maisha yake kiuchumi, kwa kumpa uwezo wa kujenga nyumba ya gorofa, kuinvest kwenye studio pamoja na hela nyingine ndefu kubaki mfukoni.
Mpaka mara ya mwisho anaongea na millardayo.com Jua Cali ambae alikiri kupunguza safari za kupita katikati ya Nairobi kutokana na tishio la mabomu ya Al Shabab, alikua anamiliki gari aina ya Noah.
Facebook comments for blogger brought to you by Eddie sucre?
No comments:
Post a Comment