Thursday, August 23, 2012

KARUDI KIVINGINE NI MWENDO WA RED CAPERT

 
msanii aliewahi kufanya vizuri sana na wimbo wake wa kwanza kabisa (uwe wangu), uliompa mashavu yakutosha mikoa tofauti tofauti miaka minne iliyopita, amechonga na blog hii baada ya kumtafuta na kutaka kujua kulikoniiiiii?
licha ya kukaa muda wote huo kimya kumbe ana ngoma kadhaa ambazo ameshazikamilisha lakini management yake bado haiko tayari kuachia pini hizo huku akisema hajui ni kwanini haziachiwi
"sijui labda wanaona bado so siwezi kujua" amesema Maunda
kwa hivi sasa anafanya movie na mpaka sasa ameshafanya movie zaidi ya mbili, moja iko mbioni kutoka wakati wowote kuanza hivi sasa, inaitwa Room number 13, iliyo chini ya kampuni ya ZG iliyopo Zanzibar, akiwa amecheza kama Ghost.

No comments:

Post a Comment