Na Haruni Sanchawa/GPL
RAIA
mmoja wa Bulgaria, Petez Ninkov, 32, (pichani) amenusurika kuuawa baada
ya kudaiwa kuiba fedha katika mashine ya kuchukulia fedha (ATM) jijini
Dar es Salaam.Tukio
hilo lilitokea hivi karibuni katika Benki ya Standard Chartered, Tawi
la Ilala ambapo mzungu huyo aliponea chupuchupu kupigwa baada ya
kuokolewa na polisi ambao walikuwa doria na haraka wakamkimbiza polisi.
Habari
ambazo tumezipata zinaeleza kuwa, tayari amepandishwa kizimbani katika
Mahakama ya Wilaya ya Ilala kujibu mashitaka ya kuiibia benki hiyo fedha
taslimu shilingi milioni 35.
Ninkov amefikishwa katika mahakama hiyo kujibu shitaka hilo la wizi katika benki hiyo tawi la Ilala jijini Dar es Salaam. Mwendesha mashitaka wa serikali, Aidah Kisumo alidai mahakamani hapo kuwa mshitakiwa alitenda kosa hilo kati ya Februari 6 na Aprili 4 mwaka huu.
Ninkov amefikishwa katika mahakama hiyo kujibu shitaka hilo la wizi katika benki hiyo tawi la Ilala jijini Dar es Salaam. Mwendesha mashitaka wa serikali, Aidah Kisumo alidai mahakamani hapo kuwa mshitakiwa alitenda kosa hilo kati ya Februari 6 na Aprili 4 mwaka huu.
Ilidaiwa
mahakamani hapo kuwa, kati ya siku hizo mtuhumiwa aliiba Dola za
Kimarekani 23,000 kutoka katika mashine ya kuchukulia fedha (ATM), mali
ya Benki ya Standard Chatered huku akijua kuwa ni kosa.
Katika
shitaka la pili Mwendesha mashitaka alidai kuwa, mtuhumiwa aliiba tena
Mei 17, mwaka huu katika benki hiyo baada ya kupanga njama ya kutenda
kosa hilo.
Hakimu
anayesikiliza kesi hiyo, Tarsila Kisoka aliiahirisha kesi hiyo hadi
Juni 6, mwaka huu na mshitakiwa ametupwa rumande baada ya kushindwa
masharti ya dhamana ambayo ni kuwa na wadhamini wawili wanaotambuliwa na
serikali ambao watasaini nusu ya mali iliyoibiwa.
Akizungumzia
tukio hilo jana kwa njia ya simu, Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum Dar
es Salaam, Suleiman Kova alisema ni lazima benki kuwa waangalifu kwa
kuwa mbinu zinazotumika kwa wizi huo ni za kisasa. Ametoa wito kwa
wananchi kutoa taarifa polisi wakimtilia shaka mtu yeyote aliye katika
mashine za ATM.
Facebook comments for blogger brought to you by Eddie sucre?
No comments:
Post a Comment