Kwenye tuzo za VMA za MTV zilizotolewa hivi karibuni Chris Brown na Rihanna walionekana wakikiss kitendo kilichofanya wengi walioshuhudia wabaki na maswali tu kwa kinachoendelea kwa mastaa hao.
Ni siku chache tu zimepita toka Rihanna alipomwambia mtangazaji maarufu Oprah kwenye show ya Tv Marekani kwamba Chris Brown atabaki kuwa mpenzi wa maisha yake, na sasa inaonekana wawili hawa kwa sasa wanazaidi ya urafiki na hiyo ni baada ya kupigana busu kwenye stage wakati utoaji tuzo ukiendelea.
Mtandao wa Global Grind umeripoti kwamba inaaminika Mpenzi wa sasa wa Chri Brown ambae ni Karrueche alikua hataki Chris aende kuhudhuria utoaji wa tuzo hizo na hata Chris mwenyewe alikua hajui kama atakwenda mpaka dakika ya mwisho ndio akakurupuka.
Stori za chinichini kwa longtime sasa hivi zimeamplfy kuhusu kuendelea kwa uhusiano wa kimapenzi lakini wa siri kati ya mastaa hawa wawili wa muziki duniani ambao walishatengana kimapenzi baada ya ugomvi kutokea.
Huyu ndio mpenzi wa Chris Brown. |
Hata hivyo haijulikani kama tukio la Chris Brown na RiRi lilipangwa ili kuzifanya hizo tuzo ziongelewe sana, nakumbuka tuzo zilizopita za EMA MTV kuna jamaa alipanda kwenye stage akiwa kama alivyozaliwa na ni tukio ambalo liliongelewa sana na likafanya hizo tuzo kuwa kwenye headlines kwa muda kitu ambacho kiliaminika kupangwa pia kwa sababu hakuzuiwa kupanda kwenye stage na aliwapita walinzi waliokua wakimuangalia tu na kama vile haitoshi akahojiwa pia hapohapo.
Wengi wanaamini matukio kama haya yanapangwa ili kuzifanya tuzo kuongelewa sana, pia kuweka alama kwenye kumbukumbu za watu ili hata tuzo nyingine zikitangazwa idadi kubwa iangalie kwa shauku kwamba wakati huu kitatokea kituko gani.
Facebook comments for blogger brought to you by Eddie sucre?
No comments:
Post a Comment