Tuesday, October 2, 2012

TID A.K.A ZE MNYAMA ATAFANYA VITU VYAKE NDANI YA FIESTA 2012 DAR CITY ....BAADA YA KUMISS SHOW KIBAO!!!!


Baada ya miaka mitano bila kupata nafasi ya kupanda kwenye stage ya show za Fiesta, hatimaye Top in Dar, TID, atapanda kwenye show ya kilele cha tamasha hilo la kila mwaka, litakalofanyika October 6 kwenye viwanja vya Leaders, jijini Dar es Salaam.

Hiyo inamaanisha kuwa TID ambaye siku za hivi karibuni amekuwa akijiita ‘Mnyama’ atashare stage moja na Rick Ross.



”Kinondoni+Fiesta+MNYAMA is equal to ‘Mtama wa Shingo’…..BHAAAASS!!!! Watoto WadoGO WAMEKWISHA", ameandika TID ambaye jina lake ni Khalid Mohamed kupitia Facebook.

Kupitia XXL ya Clouds FM, watangazaji wa kipindi hicho wamesikika wakimtaja TID kama msanii rasmi atakayetumbuiza kwenye show hiyo.


Hivi karibuni kupitia ukurasa wake wa Facebook, hitmaker huyo wa  Kiuno alitoa malalamiko yake kwa kutokuhusishwa kwenye show hiyo kwa muda mrefu.


“I wish I coUld maKe the Guy Who does the FIESTA Listing be oN my SiDe some PeoplE are workin verY Hard to juSt makE me Look like Criminal so I can not be on List Lakini Mungu atanipa Better than Fiesta tho its Been 5 years am nt Part of It,aliongezea

No comments:

Post a Comment