Tuesday, November 13, 2012

Snura akana yeye Sio Msagaji




http://4.bp.blogspot.com/-XaTj7AJgyE8/UJ5fkHoiLAI/AAAAAAAAVG8/nqpGajlot0s/s1600/snura1.jpg
 Snura

 Snura Mushi, Jaqueline Wolper,Wema Sepetu
 Msanii wa kike katika tasnia ya filamu Nchini, Snura Mushi ‘Snura’ amekanusha kuhusika na kashifa inayomwandama kuwa yeye ni msagaji, msanii huyo anasema kuwa katika mambo yanayomnyima raha katika maisha yake ni huo uvumi unasambazwa na adui zake kuwa yeye ni msagaji wakati yeye hana tabia hiyo katika usichana wake.

“Sina kabisa tabia ya usagaji wala sijui kama kuna mchezo kama wa aina hiyo nasema kutoka moyoni mimi si msagaji kabisa ni mwanamke mwenye hisia kama wanawake wengine ambaye nikijaliwa naweza kuolewa

na kuwa mke mwenye familia yangu sina hayo mambo ya ajabu ajabu,”
alifunguka Snura.

Hivi sasa kumekuwa na kashifa zinazowaandama wasanii wa kike wa filamu kwa kuwa na mahusiano ya wao kwa wao yaani kusagana, pamoja kuvuma kwa kashifa au taarifa hizo hadi sasa kila msanii husika anapohojiwa kuhusu suala hilo ukana na kuruka hatua mia, pengine wasanii wetu wanaiga tabia za wasanii wa nje lakini ukweli wa jambo hili unabaki kwao.
Ndo hvyo ukiwa msanii lazima majanga yakukute .... ukuzingatia kioo cha jamii ndo hatari hatari utakimulika juani na mwanga wake wa kuhumiza ni nyumbani utokapo.. wazazi ndo huwa wanapata shida zaidi.

No comments:

Post a Comment