katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo leo wameudhibiti uwanja wa ndege wa kimataifa wa Goma, baada ya mapambano makali yanayoendelea kati ya waasi na vikosi vya jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo.
Hali hiyo imetokea wakati ambao Rwanda inavituhumu vikosi vya jeshi la Kongo vinavyoungwa mkono na Umoja wa Mataifa kwa kulishambulia eneo lake wakati wa mapambano na waasi karibu na eneo la mpakani hapo jana.
Msemaji wa kundi la M23, Kanali Vianney Kazarama ameliambia shirika la habari la AP kwa njia ya simu kwamba sasa waasi wanapambana kuudhibiti mji wote wa Goma, baada ya kufanikiwa kuudhibiti uwanja wa ndege na kwamba sasa wako ndani ya mji wa Goma.
Akizungumza leo na DW, Mbunge wa jimbo la Kivu Kaskazini, Mayombo Omary Bin Fikira amethibitisha kwamba waasi wameutwaa uwanja huo wa ndege. Mbunge huyo anasema kwa sasa hali ni ya kutatanisha katika mji wa Goma na milio ya risasi imekuwa ikisikika.
Rwanda haina mpango wa kulipiza kisasi

Rais Joseph Kabila na Rais Paul Kagame
Aidha, mbali na Rwanda kuishutumu Kongo, imesema haina mpango wa kulipiza kisasi kwa kile ilichokiita uchokozi unaofanywa na Kongo. Waziri wa Mambo ya Nje wa Rwanda, Louise Mushikiwabo ameliambia shirika la habari la Reuters kuwa masuala ya mashariki mwa Kongo ni nyeti na hayapaswi kufanyiwa mchezo.
Awali msemaji wa jeshi la Rwanda alisema jeshi la Kongo liliushambulia mji wa mpakani wa Gisenyi na kuwajeruhi watu watatu, wakati mapigano yalipokuwa yanaendelea kati ya jeshi la Kongo na waasi wa M23 waliokuwa wakiukaribia mji mkuu wa mkoa wa Kivu Kaskazini wa Goma.
Serikali ya Kongo ambayo imerudia kuishutumu Rwanda kwa kuwaunga mkono waasi wa M23, katika harakati zake za kudhibiti madini Kivu Kaskazini. Msemaji wa serikali ya Kongo, Lambert Mende amesema wana taarifa kuwa Rwanda imekuwa ikifyatua risasi kwenye himaya yake yenyewe ili kuhalalisha uvamizi mkubwa unaoufanya.
Umoja wa Mataifa waendelea kuishutumu Rawanda

No comments:
Post a Comment