Dk Shukuru Kawambwa. Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Matokeo hayo mapya yanaonyesha kuwa, ufaulu wa kuanzia daraja la kwanza hadi la nne umeongezeka kutoka asilimia 34.5 kwa matokeo yaliyotangazwa awali na kufikia asilimia 43.08. Hii inamaanisha kwamba watahiniwa wapatao 30,063 ambao awali walikuwa wamepata sifuri katika matokeo ya awali sasa wamepanda na kupata madaraja ya ufaulu katika matokeo mapya. Matokeo ya awali yaliyotangazwa na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk Shukuru Kawambwa yalionyesha kuwa kati ya watahiniwa 367,756 waliofanya mtihani wa kidato cha nne mwaka jana, waliokuwa wamefaulu kwa daraja la kwanza mpaka la tatu walikuwa 126,847 sawa na asilimia 6.4. Waliopata daraja la nne walikuwa ni 103,327 sawa na asilimia 28.1. Katika matokeo hayo, watahiniwa 240,909 sawa na asilimia 65.5 walipata sifuri, hesabu ambayo imebadilika katika matokeo mapya ambayo yanaonyesha kuwa sasa waliopata daraja hilo ni 210,846 sawa na asilimia 56.92 wakati wavulana wakiwa ni 104,259 na wasichana 106,587. CLICK HAPA UPATE MATOKEO |
Facebook comments for blogger brought to you by Eddie sucre?
No comments:
Post a Comment