Friday, February 21, 2014

Now you know why Facebook bought Whatsapp

Kampuni ya Facebook imenunua kampuni ya Whatsapp kwa malipo ya thamani ya dola bilioni 16.

Hata hivyo kununuliwa huko kwa Whatapp hakumaanishi kuwa Whatapp itaacha kufanya kazi, bali kampuni ya Facebook na Whatsapp zimesisitiza kuwa huduma itaendelea kubaki kama kawaida.
Kinachotokea ni kuwa wafanyakazi wa Whatsapp wanakuwa wafanyakazi wa Facebook na huduma hiyo ya Whatsapp itatambulika kuwa ni mali ya Facebook.
Watalaamu wa biashara toka Forbes.com wanadadisi kuwa hii ni moja ya mbinu ya Facebook kuua ushindani wa mitandao mingine ya kijamii ambayo inaonekana kuwa tishio kwani Facebook ina watu wenye akaunti takriban bilioni 1.2 wakati Whatsapp ina watumiaji karibu nusu bilioni, na imekuwa ikikua kwa kasi siku hadi siku.
--Kumbuka kuwa Facebook ilinunua huduma ya INSTAGRAM kwa dola za kimarekani bilioni 1, wakati huo INSTAGRAM ndio imepamba moto kweli kweli.
--Lingine la kukumbuka ni kuwa INSTAGRAM ilinunuliwa wakati ndio kwanza ina miezi 18 toka ianzishwe, wakati Whatsapp yenyewe imenunulia ikiwa na miaka 5 toka ianzishwe. Yaani huduma zote hizi zilikuja baada ya FB kuanzishwa ila zimekuwa tishio kwa FB.
--Habari hii imeripotiwa na vyombo vya habari vya BBC, CNN, Business Insider, Blomberg na Facebook wenyewe.

No comments:

Post a Comment