Monday, January 28, 2013

Mwanamke mwenye hipsi kubwa duniani

 

LOS ANGELES, Marekani
WAKATI wanawake wengi duniani wakihangaika kukuza ukubwa wa makalio yao, huku wengine wakitumia njia ya kuvaa taiti zenye hipsi, wanaume wengi huko mjini Los Angeles wamejikuta  wakigeukageuka kumwangalia mwanamke mwenye makalio makubwa kupita kiasi kila apitapo njiani.
Mikel Ruffinelli ni mwanamke ambaye mpaka sasa ‘ameishavunja shingo’ za wanaume wengi. Makalio yake na hispi zake za asili zimemfanya atawazwe kuwa mwanamke mwenye hipsi kubwa kuliko wanawake wote duniani.
Mikel anayeishi nchini Marekani hajatumia dawa za mchina wala dawa zozote kama wafanyavyo akina dada wengine na ndiye aliyetambulishwa kuwa ndiye mwanamke mwenye hipsi kubwa kuliko wanawake duniani. Mpaka sasa mama huyo mwenye familia yake ana  hispi zenye  mita 2.44.
Umbile lake halikuja hivihivi, bali alikuwa ni mtu mwenye umbile la kawaida, licha ya kukiri kuwa ndugu zake wengi wana maumbile makubwa.
Hipsi za mwanamama huyo zimekuwa zikiongezeka siku baada ya siku kadiri alivyokuwa akijifungua watoto wake.
Mikel Ruffinelli, ambaye ni mama wa watoto wanne ana umri wa miaka 39 na ni mkazi wa Los Angeles amejisifia kuwa umbile lake limekuwa likiwachanganya wanaume wengi.
Akiwa na kiuno kidogo kisichoendana na mwili wake cha inchi 40, hispi zake zina mzunguko mkubwa wa inchi 96.
“Nalipenda umbile langu na sina mpango wa kujikondesha kwa diet,” alinena Mikel na kuongeza kuwa wanaume wengi wanapenda wanawake wenye maumbile makubwa siyo wale wembamba wembamba.”
Lakini kauli hiyo, imepingwa vikali na Jennifer Lopez, Kim Kardashian na Beyonce ambao wanasema inategemea na mwanaume husika na namna kile anachokipenda, lakini wakati mwingine hutegemea na mazoea ya mwanamume.
Mikel pamoja na kutamba na maumbile yake hayo ambayo anadai ni urithi toka kwenye familia yake ambapo karibuni ndugu zake wote wa kike nao wana hispi kubwa.
Mikel amelazimika kuishi tofauti ili aweze kuendana na umbile lake, hawezi kuenea kwenye gari ndogo hivyo gari analoliendesha ni kama lori.
Akiwa nyumbani kwake inabidi akae kwenye makochi yaliyotengenezwa kwa chuma badala ya mbao, pia kitanda chake nacho ni futi saba kwa saba.
Mume wa Mikel, Reggie Brooks mwenye umri wa miaka 40 ameelezea kupagawishwa na umbile la mkewe na ameongeza kuwa kila siku humsifia kwa kumwambia jinsi gani alivyo mrembo.
Mikel na mumewe wapo kwenye ndoa kwa miaka 10 sasa na wamefanikiwa kupata watoto watatu ambapo mtoto wa kwanza wa Mikel alizaliwa katika ndoa yake ya kwanza kabla hajaachika na kuolewa na Reggie.
 chanzo mwananchi

No comments:

Post a Comment