Hatimaye
tumepata jibu la kwanini Judith Mbibo aka Lady Jaydee amekuwa akitweet
vitu vizito weekend iliyopita. Kama hukufaniwa kuziona tweets hizo ni
kwamba mwanadada huyo alishusha mfululizo wa mabomu kuelekea kwa kituo
kimoja cha radio na kujikuta akiongeza aka mpya, Anaconda.
Na
sasa imebainika kuwa mwanamuziki huyo mkongwe na mjasiriamali anakuja na
kituo chake cha radio kiitwacho Kwanza FM. Habari hiyo aliibreak
mwenyewe jana na bila shaka haihusiani na April’s Fools Day.
Kwanza FM coming soon. Yangu mwenyewee
— Lady JayDee (@JideJaydee) April 1, 2013
Inaonesha
kuwa mchakato wa kuanzisha radio hiyo unaenda vizuri kiasi cha kuweka
wazi na kuwa hiyo ndio sababu alichukua uamuzi huo wa kuandika mambo
ambayo yangeweza kuiharibu career yake ya muziki.
Huwezi kuanza mapambano km hujajizatiti, si utapigwa ufe.? Vita ni pale tu unapokuwa tayari. Sikuwa tayari huko nyuma ndio maana sikuongea
— Lady JayDee (@JideJaydee) April 1, 2013
Kila
lakheri Lady Jaydee. Kwa usimamizi wa mumewe Gadner G Habash ambaye ana
uzoefu mkubwa kwenye masuala ya radio, kituo hicho huenda kikafanya
vizuri.
Facebook comments for blogger brought to you by Eddie sucre?
No comments:
Post a Comment