Sunday, August 12, 2012

AY NA SAFARI YA MAREKANI.

 Naona siku zinahesabika na zimebaki chache kwa ajili ya Ay kuchukua pipa moja kwa moja mpaka Los Angeles Marekani kwa ajili ya kufanya ile project kubwa ambayo kila alieisikia taarifa yake zaidi ya mwaka mmoja uliopita amekua na hamasa ya kusikia nini kinaendelea.

Mwimbaji Staa Sean Kingston alipokuja bongo mwaka juzi alitangaza kupitia XXL ya CLOUDS FM kwamba yuko tayari kufanya kolabo na Mtanzania Ay ambapo siku kadhaa mbele, Ay alinisikilizisha wimbo wake aliorekodi Marekani ambayo ndio kolabo na Sean Kingston.

Ulipita muda wa ukimya kidogo baada ya Ay kurekodi audio ya kolabo ya kwanza na Kingston ambayo ndio alinisikilizisha, ukimya ulifata baada ya hapo lakini kumbe Ay alikua anavuta subira na kuongeza uvumilivu kutokana na ratiba nzito ya Kingston ambae alikubali kufanya nae kolabo bure, wakati Jose Chameleone wa Uganda kwenye kolabo aliyoahidiwa na Sean Kingston ameambiwa atailipia USD elfu 30 ambazo ni zaidi ya milioni 45 za kibongo.

Ay amesema “Marekani nakwenda September 2012 kufanya kolabo na Tyga wa Cash Money pamoja na video na Sean Kingston, hizi kazi zinahitaji hela lazima uwe unajipanga kwelikweli yani ukienda unafanya kazi unamaliza unarudi zako”

No comments:

Post a Comment