Sunday, August 12, 2012

WEMA KUTOKA TENA NA DIAMOND KIMTINDO...!

Kutokana na hali ya afya ya msanii nyota kwenye tasnia ya muziki wa Bongofreva Naseeb Abdul ‘Diamond’ kutetereka hali hiyo imechangia kushindwa kuchukua matukio ya ujio wa filamu yake iliyokuwa inatarajiwa kuanza kurekodiwa hivi karibuni 

Kwa mujibu wa mtayarishaji wa filamu hiyo Selles Mapunda amefunguka kwa kusema kuwa kuumwa kwa msanii huyo kumefanya kuharisha kuchukua picha kwa ajili ya ujio huo . “Hali ya msanii huyo inaendelea vizuri na tunatarajia hali itazidi kuwa nzuri na atakapopona tutaanza rasmi uchukuaji wa picha hizo” alisema mapunda 

Kama ilivyokuwa kwenye filamu ya Crazy Tenant aliyoigiza msanii Peter Msechu, Mapunda aliongezea kuwa ujio wa filamu hiyo ulikuwa unatabili na Diamond filamu hiyo ilipewa jina la ‘Nimpendenani’kutokana na ngoma yake iitwayo jina hilo kufanya vyema 

Hata hivyo mwaandaaji wa filamu hiyo amedodosa kuwa katika filamu hiyo Diamond ambaye ni muhusika mkuu ataigiza na muigizaji mmoja wapo kati ya Wema Sepetu au Jokate Mwigelo 

No comments:

Post a Comment