Mkurugenzi wa Machozi Entertainment, Gadna G. Habash.
MACHOZI ENTERTAINMENT
Press Release
Miss Ilala 2012
KAMATI ya maandalizi ya shindano la Miss Ilala 2012,
kesho Alhamis saa 5 asubuhi, itatambulisha mbele ya wanahabari warembo
15, wanaowania umalkia wa taji hilo, linaloshikiliwa na Vodacom Miss
Tanzania, Salha Israel.
Warembo hao kutoka vitongoji vya Dar City Center,
Tabata na Ukonga wamekuwa katika kambi hiyo kwa wiki mbili sasa na
wamekuwa wakiendelea na mazoezi katika Club ya Nyumbani Lounge, iliyopo
maeneo ya Namanga, Dar es Salaam sehemu ambayo kesho itatumika katika
hafla hiyo fupi ya utambulisho.
Miss Ilala 2008, Slyvia Mashuda ndiye mkufunzi wa
warembo hao na ikumbukwe Slyvia alishika nafasi ya pili katika Miss
Tanzania mwaka ambao Nasreen Karim alitwaa taji la Miss Tanzania.
Wadhamini waliothibitisha katika mashindano hayo ni
pamoja na City Sports Lounge, gazeti la Jambo Leo, Nyumbani Lounge,
100.5 Times FM, Uhuru One na 88.4 Cloud's FM na Redds Premmium Cold.
Miss Ilala 2012 Itafanyika Septemba 7, mwaka huu katika sehemu ya nje ya
Nyumbani Lounge.
Natanguliza shukrani, wanahabari wenzangu
Gadna G. Habash
Mkurugenzi Machozi Entertainment |
No comments:
Post a Comment