Thursday, October 18, 2012

DIAMOND ANATAMANI KURUDI CLASS


 
 Kasumba ya kutafuta maisha kwa kujiendeleza kielimu msanii huyu afunguka kwa kuonyesha umuhimu wa kuwa na elimu ya darasani na nia yake ya dhati hayo yameelezwa na...

Nasseb Abdul ‘Diamond’, amedai kuwa anatamani kurudi shule kuendelea na masomo lakini kutokana na shughuli zake za muziki anakosa nafasi.

Akiongea na mwandishi wetu alidai kuwa anaamini elimu yake ya kidato cha nne ni ndogo sana na ana changamoto nyingi ili kufikia level za kimataifa, hivyo ana mipango ya kurudi shule lakini akifikilia mambo mengi muziki na ratiba za show huwa anakata tamaa kabisa lakini anaamini atafanya hivyo siku moja ili kutimiza ndoto yake ya kufika mbali zaidi kielimu.

Diamond alisema kuwa kuna umuhimu wa yeye kwenda shule lakini kwa sasa hafikirii kama anaweza kukaa tena darasani na kumsikiliza mwalimu pengine aende nje kwa ajili ya kusomea muziki huku akiendelea na kazi hiyo hata huko atakapokuwa akisoma.

“Naweza kurudi shule lakini pengine nikasomee muziki na mambo mengine yanayohusu muziki,”
akiongezea

No comments:

Post a Comment