Monday, October 29, 2012

HATIMAYE TRENI ILIYOKUWA IKISUBILIWA KWA HAMU DAR YAANZA KAZI RASMI

Leo baadhi ya wakazi wa jiji la Dar-es-Salaam wameanza rasmi matumizi ya usarifi wa kutumia treni.

Haya ni maoni ya Wananchi juu ya huduma hiyo ambayo itaenda kukata mzizi wa FITINA kati ya makonda na Wananchi


Muda mwingine tuwe wakweli japo tuna itikadi tofauti...Serikali ya awamu hii imejenga Machinga Complex,Imejenga madaraja makubwa ma4 mawili kati ya hayo ni makubwa kama lile lilojengwa awamu ilopita madaraja hayo ni Malagarasi,Kigamboni,kilombero na lingine moja jina nimesahau limetoka kuzinduliwa week ilopita,Pia barabara nyingi za kata za lami na zile za changarawe,imezindua usafiri wa reli,Imeanza kuboresha barabara kuu zilizokuwa za njia 1 kuwa za njha 2 na nyingine 4 hapa nazungumzia barabara ya Old Bagamoyo kuanzia mwenge Tegeta,Bunju na kuendelea.Barabara 4 ni Morogoro road..

Nawapongezeni saana akina mwakyembe na viongozi wengine waige mfano wao


Naipongeza serikali kwa ujumla maana haya ndio mambo ambayo tulitalajia, Kama wametimiza hatuna budi ya kuwashukuru. Mimi binafsi nawatakia mafanikio ktk yote waliyoyapanga kuyafanya

Nihatua moja wapo tz tumepiga japo kwa wenzetu hilo ni jambo dogo sana.

big up to harrison mwakyembe.


 kwanza pongezi kwa mh.Mwakyembe kwa juhudi zake,kingine waongeze mda wa kazi angalau mpaka saa 2200 usiku,bado wa2 wanakuwa wanatoka makazini


Hapo sasa dar washindwe wenyewe tu..? Ni vizuri kwa hilo naipongeza serikal, tu.. Je ni lini huduma ya MAJI ITAKUWA BURE HAPA Tanzania maana tunalipa kodi zetu na hatujui wap zaenda akhasante sana .

 Hongera Sana Mwakyembe.Well done! 2015 Tutakupa Jembe la ukweli Dr.W.Slaa na wewe ukiwa waziri wake mkuu.(Dr.Slaa Mwakyembe Magufuli Sita namajembe yetu mengine Duh! Hakika nchi yetu Itakaa pazuri sana.Anyway Tumwombege Mungu awafungue macho baadhi ya akinamama na wazee walokomaa kumshikilia mdudu Dumuzi anayewalia mazao yao wao wenyewe.Nisawa na kumfuga chatu chumbani.Kifupi nchi imeuzwa na ninawasiwasi na Raia kama hatujauzwa,Sie tunajua tunaishi kama raia kumbe wenze wametufanya bidhaa.Waulaya wakifika bei tunakabidhiwa.Our Beutiful country Dunia nzima wanaitamani tusimame kwa pamoja tuzilinde laslimali zetu.


 Kwa leo naomba nikupongeze tu Mh. MWAKYEMBE kwani ulichokifanya ni ukombozi kwa wenye hali ya chini!!! Mungu azidi kukupa afya njema!!


 HATA kama mtasema mlianza, inawezekana mngeshindwa mwishoni, hongera mwakyembe


 ni mzuri lakini serikali ifikirie kupunguza nauli kuwa sawa na ile ya daladala au chini ili kufanikisha malengo ya matumizi ya treni kwa watu wote


mda wa hii mashine kuondoka ni saa ngapi?


we thank for the good start but we need the progress more and to advance in technology.Ni nzuri sana,ila naomba niwaase watanzania wenzangu tujenge utamaduni wa kupenda na kuthamini vitu vyetu kwa kuvitunza na kumea wale wote watakaotaka kuviharibu mbele yetu,nikiangalia hzo seats hapo zinaonekana ni nzuro na zinavutia sana,lkn nina mashaka sana baada ya wk mbili au mwezi mmoja ztakuwa zimechorwachorwa eti kisa watu wanataka kuacha kumbukumbu,huo ni ujinga na ulimbukeni kama unataka kuacha kumbukumbu buni kitu au anzisha kitu ambacho kinakufanya ukumbukwe maisha yako yote uwe mzima au mfu na cyo kuchafua na kuharibu mali za Umma kama hyo tren nzuri inayoonekana hapo,Hongera sana Mh.Mwakyembe na timu yako zima kwa jitihada zako za kupunguza adha ya usafiri katika Jiji la Dar es salaam,Mungu akuzidishie hekima na busara uweze kubuni njia nyingine za kupunguza adha ya usafiri.


Chanzo vodacom page




No comments:

Post a Comment