Monday, October 29, 2012

SITAISAHAU FACEBOOK

SITAISAHAU facebook

Niliuchukia umasikini, nikautamani utajiri wa haraka haraka.
Sikuyajua madhara ya kula vya bure.
Nilijiona mimi ndiyo mimi hakuwepo wa kufananishwa nami, pesa za bwelele zikanipa kiburi, nikawa sikamatiki.

Mambo yaliponibadilikia, nilitamani dunia inimeze.
Zile pesa zikaanza kunipa suluba. Mateso juu ya mateso.
Nikadhalilika, Nikafedheheshwa na kuaibika.
Zile pesa za maajabu zikanitokea puani........!
Nikailaani facebook kwa kunikutanisha na rafiki wa maajabu.........

***NI KIPI KILIMSIBU MWANADADA HUYU MWANAFUNZI WA CHUO KIKUU CHA MT. AUGUSTINO MWANZA......Mimi sijui kwakweli..kila kitu ndani ya kitabu hiki cha kustaajabisha cha Sitaisahau facebook.
Kimetungwa na mwanadada Emmy John Pearson....kipo tayari wasiliana naye kwa namba 0654 960040 akuelekeze utakipata vipi....

USIKOSE. Huenda nawe UNATUMIKIA MWANADAMU bila kujitambua.
hawa ni baadhi ya watu waliofanikiwa kupata simulizi hili la haina yake

Ama kweli ukiwa katikati ya warefu ndo utagundua kuwa wewe ni mfupi.
# Hapa nikiwa na rafiki zangu...Dee Dion na Hansy Mansour......mkononi kitabu cha simulizi matata ya mwanadada Emmy John Pearson......SITAISAHAU facebook.......


No comments:

Post a Comment