Friday, October 26, 2012

MISS TANZANIA AVAMIWA USIKU, ILIBAKIA KIDOGO WASEPE NA MKOKO WAKE



WATU wanaosadikiwa kuwa ni majambazi juzikati walivamia nyumbani kwa Miss Tanzania 2011, Salha Israel maeneo ya Sinza-Mori jijini Dar na kufanya jaribio la wizi.


Miss Tanzania 2011, Salha Israel.
Akizungumza na Ijumaa, Salha alisema tukio hilo lilijiri hivi karibuni mishale ya saa 8:00 usiku ambapo watu hao wasiofahamika waliruka ukuta na kutaka kufanya uhalifu lakini walishitukiwa kabla ya kutekeleza mpango huo.
“Sijui niseme ni wezi au majambazi ila ilikuwa saa 8 usiku, watu hao waliruka ukuta wakaingia ndani. Hutujui kama walitaka kuondoka na gari au kuiba vitu vilivyokuwemo ndani yake lakini walivunja kioo cha mbele.
“Kwa bahati tulisikia vurugu zao na kabla ya kuiba chochote, tuliwakurupusha na ndipo walipokimbia,” alisema Salha.

No comments:

Post a Comment