Tuesday, November 27, 2012

Wasanii wa Bongo Flava wanatengeneza nyimbo ya kumkumbuka Sharo millionare

Gari aliyopata  nayo ajari Sharo Milllionare  jana Mida ya saa 2 usiku Tanga, 
Yanayojiri kwenye msiba wa Sharo Milionea: Hali ya mzee King Majuto presha imepanda na hali kuzidi kuwa mbaya kutokana na kupata taarifa za msiba wa Sharomilionea.

Mjomba wa marehemu Sharo milionea, Bwana Omary Fundikira asema marehemu ana
tarajiwa kuzikwa hapo jumatano siku ya kesho hii ni kutokana na msanii mwenzake John Maganga kuzikwa leo.

Mkuu wa polisi mkoa wa Tanga RPC Costantine Massawe asema Hussein Ramadhani (Sharo milionea ) alikuwa mwenyewe katika gari na ilipotokea ajali gari lilimrusha nje na kufariki hapohapo.

Pia rafiki wa marehemu bwana Mohamed Ismail ambaye ndiye aliyemuazimisha gari alilopata nalo ajali, asema ilitakiwa waongozane kwenda Tanga pamoja ila alishindwa maana alipata majukumu mengine.

Hawa ndo wasanii watakao tengeneza nyimbo MAALUMU
#RichMavocal, #Barnaba, #Shilole, #Dayna #Stamina na wasanii wengine wako #KiriRecords sasa wakirekodi wimbo maalumu kwa #SharoMilionea
 

No comments:

Post a Comment