Amatus Liyumba akielekea kusikiliza kesi yake katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar
ASKARI wa Jeshi la Magereza mwenye namba F. 3251 Staff Sajenti Magesa leo alifika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam kutoa ushahidi katika kesi ya kukutwa akitumia simu gerezani inayomkabili Mkurugenzi wa Utawala na Utumishi wa zamani wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Amatus Liyumba.
Hata hivyo Magesa alishindwa kutoa ushahidi wake baada ya kesi hiyo kuahirishwa kufuatia wakili wa Liyumba, Majura Magafu kupatwa na dharura. Shahidi huyo anatarajiwa kutoa ushahidi huo Januari 17 mwakani kesi itakapotajwa tena mahakamani hapo.
Facebook comments for blogger brought to you by Eddie sucre?
No comments:
Post a Comment