Thursday, August 9, 2012

JB kama kawaida kujisifu





MWIGIZAJI na mtayarishaji wa filamu anayeongoza kwa mauzo ya filamu za Swahiliwood kwa sasa, Jacob Stephen �JB�, amewashukru Watanzania kwa kupenda kazi zake zinazopokewa vizuri kila kukicha.

Anasema amekuwa akijitahidi kutowaangusha kwa kuwapa kazi bora na ndiyo maana ana uhakika wa kuendelea kufanya vizuri sokoni siku zote.

"Ni kweli hili halina ubishi kuwa mimi ni mtu nyota na mashuhuri kwa Tanzania hata Afrika Mashariki, lakini najua hilo linatokana na wapenzi wa filamu kukubali kazi zangu na kununua kazi halali," alisema.

"Hilo ndilo jambo linaloniletea mafanikio na nitazidi kufanya kazi kwa nguvu."

JB ametengeneza filamu nyingi zilizopendwa, kati ya hizo kuna 'DJ Ben', 'Senior Bachelor' , 'Nakwenda Kwa Baba' na 'Kanisa La Leo' .

No comments:

Post a Comment