Habari zilizopatikana na kuthibitishwa na mbunge aliyefungua malalamiko hayo, Charles Mwijage (Muleba Kaskazini-CCM), zinasema kuwa mbunge huyo wa Singida Mashariki kwa tiketi ya Chadema, alimkashifu.
Hivi karibuni, Tundu Lissu alizungumza na waandishi wa habari bungeni na kuwataja wabunge saba kuwa wana mgongano wa kimasilahi kwenye Kamati ya Nishati na Madini.
Wabunge hao wote kutoka Chama Cha Mapinduzi (CCM) ni Sara Msafiri (Viti Maalumu), Mariam Kisangi (Viti Maalumu), Christopher Ole Sendeka (Simanjiro), Vicky Kamata (Viti Maalumu), Yusuph Nassir (Korogwe Mjini), Charles6 Mwijage (Muleba Kaskazini) na Munde Tambwe (Viti Maalumu).
Akizungumza na Mwananchi juzi, Mwijage alikiri kumwandikia Spika wa Bunge, Anne Makinda kumlalamikia kuhusu Lissu.
“Ni kweli nimemwandikia barua Spika na nimeshaikabidhi, nataka shauri letu lisikilizwe na nitendewe haki,” alisema.
Alisema kutokana na matamshi ya Lissu, vyombo vya habari na mitandao ya kijamii ilimwandika kuwa ni mla rushwa na kuathiri hadhi yake.
Mwijage pia amelilalamikia gazeti la Tanzania Daima kuwa liliandika habari hiyo kwa kumtaja kuwa ni mla rushwa na baadaye likasambazwa jimboni kwake kwa masilahi ya kisiasa.
Kwa upande wake, Lissu alisema hajaitwa na Kamati ya Bunge kuhusu suala hilo lakini alikiri kupata taarifa hizo kutoka kwa Mwijage.
“Nimekutana na Mwijage akaniambia amenishtaki na mimi nimemuuliza ‘unajua nilichokisema?’ na yeye akaniuliza kwani ulisema nini? Nimemweleza kuwa mimi nawajibika kwa maneno yangu kuwa yeye ana mgomgano wa kimasilahi kwa kuwa consultant (mshauri ) wa kampuni ya Puma. Siwezi kumwita mtu mla rushwa kwa kuwa sina ushahidi na hilo,” alisema na kuongeza:
Facebook comments for blogger brought to you by Eddie sucre?
No comments:
Post a Comment