Thursday, August 9, 2012

Mkwere haishi vituko






ELIZABETH EDWARD
MKWERE ambaye ni miongoni mwa wachekeshaji mahiri wa Tanzania kupitia kundi la Mizengwe, amesema licha ya baadhi ya watu kumwona kituko, lakini mkewe na familia yake ina mtazamo chanya dhidi yake.

Msanii huyo ambaye ni baba wa mtoto mmoja, anasema kuwa anapata faraja kwa kuwa familia yake inamuunga mkono kwa kiasi kikubwa kwa kazi anayofanya ingawa, ipo katika mazingira magumu.

Anafafanua kuwa watu wengi wanachukulia kazi yake kama ni kituko, lakini mke wake amekuwa mwelewa na mwenye kumtia moyo ili aendelee na kazi hiyo.

�Mke wangu ni mwanamke mwelewa, anaelewa vizuri kazi yangu ingawa watu wanaona nafanya vituko, lakini yeye anajua nipo kazini,�anasema.
�Muda ninaopata nafasi ya kuwa na familia yangu napendelea kuweka vikao, kujadili mambo mbalimbali kwa kuwa mara nyingi nakuwa kwenye shughuli za kikazi.

�Watu wanadhani kuiga mambo ya kizungu ndiyo ujanja, hawaelewi kuwa hali hiyo inachangia kwa kiasi kikubwa mmomonyoko wa maadili na kuacha tamaduni zetu.

�Kwa sasa kuna kazi za sanaa zinazoangaliwa kwa rika, hiyo inatokana na mambo ya ajabu yanayooneshwa humo. Hii inasababishwa na kukosa ubunifu.

"Vijana watambue kuwa sanaa ni chanzo kikubwa cha ajira. Naweza kumudu mahitaji ya familia yangu kutokana na sanaa, hiyo inatokana na ubora wa kazi ninayoifanya."



No comments:

Post a Comment