Thursday, August 9, 2012

Wolper arudi kwa akina Massawe





JACKLINE Wolper Massawe anafikiria kurudi kwao Moshi mara baada ya kumalizika kwa Mwezi wa Ramadhan.

Si kwamba anarudi mazima, anasema anafikiria kurudi kwao kwa lengo za kufanya filamu katika maeneo ya huko kunakozalishwa mbege kwa wingi kuliko sehemu yoyote duniani.

"Baada ya kushereherekea Sikukuu ya Iddi na kupumzika kidogo, itanibidi niende nyumbani Moshi kwa ajili ya kufanya filamu," alisema.

"Maeneo ambayo nitayatumia ni ya milimani maana yana mandhari nzuri na ya kuvutia, kuhusu ni filamu gani na ngapi ambazo nitazicheza huko bado ni mapema sana kueleza, lakini 'Location Manager' wangu anayejulikana kama Lyumba ameshaenda na amekagua maeneo yote na ameshaweka kila kitu tayari."

No comments:

Post a Comment