Thursday, August 9, 2012

Ray aamua kwenda na wakati





HATA tasnia ya filamu inaweza kwenda na wakati, mwigizaji na mtayarishaji, Vicent Kigosi 'Ray' anakamilisha kitu maalumu kwa ajili ya kipindi hiki cha Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

Kwa mujibu wa Ray, filamu hiyo iliyopewa jina la 'Glory Of Ramadhan' ipo tayari inaingia sokoni leo Jumanne.

"Mzigo uliokuwa ukisubiriwa kwa hamu na wadau wa tasnia ya filamu nchini sasa unaingia mtaani, ni bonge la movie na wala si ya kuikosa. Imejaa mafunzo ya kutosha kuhusu Mwezi Mtukufu," alisema.

Ray amewataja baadhi ya mastaa waliogiza katika filamu hiyo kuwa ni yeye mwenyewe, Batuli (Neshi), Chuchu Hans na Dulla ambaye ni mtangazaji wa kipindi cha Planet Bongo.


No comments:

Post a Comment