Friday, September 7, 2012

Sweden yalaani mauaji ya Mwangosi

MWILI WA DAUDI MWANGOSI

BALOZI wa Sweden nchini Tanzania, Lennarth Hjelaker, ameungana na mamilioni ya Watanzania, kulaani tukio la kifo cha Mwandishi wa Habari wa Kituo cha Channel Ten, Daudi Mwangosi.

Amesema kuwa, kitendo cha mwandishi huo kuuawa akiwa kazini, kimeleta taswira mbaya kwa uhuru wa habari nchini.
Hjelaker aliyasema hayo jijini Dar es Salaam jana, alipokuwa akifungua mkutano mkuu wa mwaka wa Shirikisho la Vyama vya Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC).

Mkutano huo wa siku mbili ulioanza jana, umewakutanisha viongozi wa vyama vyote vya waandishi wa habari nchini na unatarajia kuhitimishwa leo.

“Natoa salamu zangu za rambirambi kwa waandishi wote wa habari, ndugu na familia ya Marehemu Daudi Mwangosi na pia naungana nanyi katika kipindi hiki kigumu,” alisema balozi huyo kwa kifupi.

Pamoja na mambo mengine, waandishi hao walitoa tamko linaloonyesha msimamo wao juu ya kifo cha Mwangosi.

Wakati akilaani mauaji hayo, Balozi Hjelaker ambaye hakuzungumza sana, alisema kwamba, Serikali ya Sweden itaendelea kushirikiana na Tanzania katika masuala ya maendeleo.


No comments:

Post a Comment