Showing posts with label matukio. Show all posts
Showing posts with label matukio. Show all posts
Sunday, October 14, 2012
Friday, September 7, 2012
Sweden yalaani mauaji ya Mwangosi
MWILI WA DAUDI MWANGOSI |
BALOZI wa Sweden nchini Tanzania, Lennarth Hjelaker, ameungana na mamilioni ya Watanzania, kulaani tukio la kifo cha Mwandishi wa Habari wa Kituo cha Channel Ten, Daudi Mwangosi.
Amesema kuwa, kitendo cha mwandishi huo kuuawa akiwa kazini, kimeleta taswira mbaya kwa uhuru wa habari nchini.
Hjelaker aliyasema hayo jijini Dar es Salaam jana, alipokuwa akifungua mkutano mkuu wa mwaka wa Shirikisho la Vyama vya Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC).
Mkutano huo wa siku mbili ulioanza jana, umewakutanisha viongozi wa vyama vyote vya waandishi wa habari nchini na unatarajia kuhitimishwa leo.
“Natoa salamu zangu za rambirambi kwa waandishi wote wa habari, ndugu na familia ya Marehemu Daudi Mwangosi na pia naungana nanyi katika kipindi hiki kigumu,” alisema balozi huyo kwa kifupi.
Pamoja na mambo mengine, waandishi hao walitoa tamko linaloonyesha msimamo wao juu ya kifo cha Mwangosi.
Wakati akilaani mauaji hayo, Balozi Hjelaker ambaye hakuzungumza sana, alisema kwamba, Serikali ya Sweden itaendelea kushirikiana na Tanzania katika masuala ya maendeleo.
Amesema kuwa, kitendo cha mwandishi huo kuuawa akiwa kazini, kimeleta taswira mbaya kwa uhuru wa habari nchini.
Hjelaker aliyasema hayo jijini Dar es Salaam jana, alipokuwa akifungua mkutano mkuu wa mwaka wa Shirikisho la Vyama vya Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC).
Mkutano huo wa siku mbili ulioanza jana, umewakutanisha viongozi wa vyama vyote vya waandishi wa habari nchini na unatarajia kuhitimishwa leo.
“Natoa salamu zangu za rambirambi kwa waandishi wote wa habari, ndugu na familia ya Marehemu Daudi Mwangosi na pia naungana nanyi katika kipindi hiki kigumu,” alisema balozi huyo kwa kifupi.
Pamoja na mambo mengine, waandishi hao walitoa tamko linaloonyesha msimamo wao juu ya kifo cha Mwangosi.
Wakati akilaani mauaji hayo, Balozi Hjelaker ambaye hakuzungumza sana, alisema kwamba, Serikali ya Sweden itaendelea kushirikiana na Tanzania katika masuala ya maendeleo.
Thursday, August 23, 2012
Tuesday, August 21, 2012
Feeding humpback whales mesmerize onlookers
Thursday, August 16, 2012
WIZARA YA FEDHA HOTUBA YA WAZIRI WA FEDHA MHE. DKT. WILLIAM AUGUSTAO MGIMWA (MB) AKIWASILISHA BUNGENI MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI YA WIZARA YA FEDHA KWA MWAKA 2012/13
Waziri wa Fedha Dk William Mgimwa
--
WIZARA YA
FEDHA HOTUBA YA WAZIRI WA FEDHA MHE.DKT.WILLIAM AUGUSTAO
MGIMWA(MB)AKIWASILISHA BUNGENI MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI YA WIZARA
YA FEDHA KWA MWAKA 2012/13
UTANGULIZI
Mheshimiwa Spika,
kufuatia taarifa iliyowasilishwa hapa Bungeni na Mwenyekiti wa Kamati
ya Kudumu ya Bunge ya Fedha na Uchumi, naomba kutoa hoja kwamba Bunge
lako Tukufu likubali kupokea, kujadili na kupitisha Makadirio ya Mapato,
Matumizi ya Kawaida na ya Maendeleo ya Wizara ya Fedha kwa mwaka wa
fedha 2012/13.
Mheshimiwa Spika, awali ya yote napenda
kutumia fursa hii kutoa pongezi zangu za dhati kwako pamoja na Naibu
Spika Mheshimiwa Job Yustino Ndugai, Mbunge wa Kongwa, Waheshimiwa
Wenyeviti Jenista Joakim Mhagama (Mbunge wa Peramiho), Sylivester
Massele Mabumba (Mbunge wa Dole) na Mussa Azzan Zungu (Mbunge wa Ilala),
kwa kuongoza vema majadiliano ya Bunge la Bajeti.
Mheshimiwa Spika, naomba nitumie
nafasi hii kuishukuru kwa namna ya pekee Kamati ya Fedha na Uchumi
chini ya Mwenyekiti wake Mheshimiwa Mtemi Andrew John Chenge, Mbunge wa
Jimbo la Bariadi Mashariki kwa maoni, ushauri na mapendekezo waliyoyatoa
kwa Wizara wakati wa kuchambua mapendekezo ya Bajeti ya Wizara ya
Fedha. Wizara imezingatia ushauri na mapendekezo ya Kamati katika
kukamilisha uandaaji wa hotuba hii.
Mheshimiwa Spika, napenda
pia kutumia fursa hii kuwashukuru Naibu Mawaziri, Mheshimiwa Janet
Z.Mbene (Mb), na Mheshimiwa Saada M. Salum(Mb) pamoja na Katibu Mkuu
Ndugu Ramadhan M. Khijjah na Manaibu wake Ndugu Laston T.Msongole,Dkt.
Servacius B.Likwelile na Ndugu Elizabeth J. Nyambibo kwa kazi kubwa
wanayoifanya ya kusimamia utekelezaji wa majukumu ya Wizara. Aidha,
nawashukuru Wakuu wa Idara na Vitengo, Wakuu wa Taasisi na Wakala wa
Serikali, chini ya Wizara na wafanyakazi wote wa Wizara ya Fedha kwa
kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi .
|
Aug 16 Tanzania opposition criticize the Govt on Mwana Halisi ban The government decision of banning Mwana Halisi, Swahili Weekly Newspaper has been questioned by the Head of Opposition Camp in the Assembly this morning.
Official Opposition Camp Head and CHADEMA Chairman, Freeman Mbowe.
The Official Opposition Camp
Leader, Mr Freeman Aikaeli Mbowe wanted to know from the Prime Minister
in a session of ‘Questions to the PM’ this morning, why the government
decided to ban Mwana Halisi while in recent days (government) has been
using court in all cases about it.
Mbowe asked if the government
does not know that it shows the signs of bad governance for passing
judgment about Mwana Halisi without involving the important governmental
pillar, Judiciary.
“Hon Prime Minister, don’t you
think that the government shows a bad sign to the growth of good
governance in the country after banning Mwana Halisi?” asked Mbowe
Responding to the question,
Prime Minister said the government uses Newspaper Act of 1976 because it
is the only law which supervises print media industry and is still in
use up to now.
“We use it because it was approved by this Assembly and is still in use. I think the decision taken was right.”
For a long time media
stakeholders have been criticizing the government for embracing the laws
such as Newspaper Act of 1976 (investing much power to the Minister)
which hinder media freedom especially to investigative stories in the
country.
|
Indian High Commissioner And Spanish
President
Kikwete commends excellent bilateral relations between Tanzania and
Spain, during his discussion with the new Ambassador of Spain to
Tanzania, Ambassador Luis Manuel Cuesta Civis at the State House in Dar
es Salaam
The
new Ambassador of Spain to Tanzania, Ambassador Luis Manuel Cuesta
Civis presents his Credentials to President Jakaya Mrisho Kikwete,
President of the United Republic of Tanzania today at the State House in
Dar es Salaam.
Wednesday, August 15, 2012
Wasiolipa Ada Kutofanya Mitihani Ya Chuo Kikuu Cha Taifa Cha Zanzibar (SUZA)
Kiongozi
wa Serekali ya Wanafunzi akimuunesha orodha ya Wanafunzi ambao majina
yao yanasubiri malipo yao kutoka Bodi ya Mkopo ya Elimu ya Juu .
Na Mwanajuma Mmanga
UONGOZI
wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA) kimezuwiya kufanya mitihani
kwa wanafunzi wote ambao hawajakamilisha ada za masomo hali ambayo
imepelekea mgongano na mizozo baina ya wanafunzi na uongozi wa chuo
hicho.
Kauli hiyo imetolewa na wanafunzi wa chuo hicho walipokuwa katika maandamano ya kudai haki yao kufanya mitihani hiyo.
Mmoja
miongoni mwa wanafunzi wa chuo hicho Ali Kombo alisema wiki moja baadae
tunatarajia kufanya mitihani hiyo ghafla wanapokea taarifa ya kuwa kila
mwanafunzi hajakamilisha malipo ya ada hatomruhusu kufanya mtihani
jambo ambalo ni kinyume na matakwa yao.
Pia
alisema kuna baadhi ya wanafunzi wanalipiwa na bodi ya mikopo la taifa
lakini mpaka sasa hawajaingiziwa fedha hizo hali ambayo inarejesha nyuma
masomo yao.
"Sisi
baadhi yetu tushalipiwa na bodi kwa asilimia 90 na kumebaki asilimia 10
tu kwanini wakatuzuilia kutofanya mitihani hiyo. hii fedha kama
asilimia 80 ishalipiwa na bodi wakati hela hiyo inakuja moja kwa moja
inaingia kwenye akaunti" alisema.
Kwa
upande wa Rais wa Serikali ya wanafunzi wa chuo hicho Ali Sharifu
Kombo, alisema kuwa yeye binafsi kwa kushirikiana na uongozi wa serikali
yake wameshafuatilia kwenye bodi ya mikopo Tanzania na kuhakikishiwa
kuwa fedha hizo tayari wameshaingiziwa.
Makamu
Mkuu wa chuo hicho Profesa Idrisa Rai alisema fedha za wanafunzi hao
bado hazijaingizwa nao kama uongozi wanalalamikia kudai ada za masomo ya
wanafunzi kwa lengo la maendeleo ya chuoni hapo.
Sambamba
na hilo Nae Kaimu Meneja wa Bodi ya Mikopo Tanzania, Patric Show
alisema fedha za wanafunzi hao tayari zimeshaingiziwa katika akaunti zao
na hivyo inawezekana ikawa ni kuchelewa kwa mawasiliano baina ya bodi
na Uongozi wa chuo hicho.
Meneja
huyo wa bodi hiyo alisema mchakato mzima uliosababisha kuchelewa kwa
kufika barua hiyo katika bodi ya mikopo Dar es Salaam kwa muhusika mkuu
ni Sajent wa bodi, lakini kumbe kabla ya hapo Mhasibu wa chuo hicho,
Rukia tayari ameshaingiziwa tokea jana.
Kutokana
na kuchelewa kwa kupelekwa kwa barua hiyo tayari zimeshaingizwa ndani
ya akaunti zao kwa kila mwanafunzi ambae yuko chuoni hapo.
Meneja
huyo amekiri kuwa fedha hizo tayari zimeshaingizwa ndani ya akaunti
hizo jumla ya shilingi milioni 13, kwa orodha ya wanafunzi 58 wa chuo
SUZA.
Hivyo
amewataka wanafunzi hao kuwa wastahamilivu katika kuvuta subra na kuwa
wasikivu kwani mipango yote ishakaa sawa na kila mmoja atapata haki yake
na atafanya mtihani huo.
Tuesday, August 14, 2012
WONDER OF THE WORLD
Is this a mosquito?
No. It's an insect spy drone for urban areas, already in production, funded by the US Government. It can be remotely controlled and is equipped with a camera and a microphone.
It can land on you, and it may have the potential to take a DNA sample or leave RFID tracking nanotechnology on your skin. It can fly through an open window, or it can attach to your clothing until you take it in your home.
Subscribe to:
Posts (Atom)