Friday, October 26, 2012

MADEE AJISEPESHA TIP TOP CONNECTION



MSANII mahiri wa muziki wa kizazi kipya anayewakilisha pande za Manzese, Hamad Ally ‘Madee’, kutoka kundi la Tip Top Connection, inadaiwa kuwa amejitoa katika kundi hilo, na sasa anataka kufanya muziki kivyake na sababu za kujitoa kwake bado hazijulikana.

Chanzo chetu cha habari kilichozungumza nasi, kwa sharti la kutotajwa kwa jina lake kilidai kuwa wiki iliyopita msanii huyo alikuwa kwenye mzozo na mmoja wa wasanii wa kundi hilo lakini waliweza kupatana ingawa jamaa bado anaonekana kutopenda kile kilichotokea lakini bado kuna vitu vingine vya ndani zaidi vilivyosabisha hadi jamaa kuamua kujiweka pembeni.

Chanzo hicho kilichopo karibu na wasanii hao hakikusita kueleza kuwa ndani ya kundi hilo kuna matatizo mengi, kwani hata kuondoka kwa baadhi ya wasanii waliokuwa hapo kulisababishwa na matatizo hayo ambayo yamemfanya Rais huyo manzese kujiengua, ingawa bado kuna mvutano mkubwa unaoendelea ili kumrudisha kundini jamaa huyo bila taarifa za mkwaruzano huo kutoka nje.

Chanzo http://http://freebongo.blogspot.com/2012/10/madee-ajitoa-ajitoa-tip-top-connection.html






No comments:

Post a Comment